[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

UPENDO AMRI MSINGI YAFUNULIWA

PDF

 

Marko 12:29-31 

29Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;

30nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

31Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

 

JUKUMU PEKEE LA MWANADAMU

Katika kucha kwa siku zake Suleimani, wakati ambapo kitani kilikuwa karibu kuvutwa juu ya mwandishi huyu maarufu wa mashairi na nyimbo, aliyejulikana pia kama mwenye hekima zaidi na utajiri mwingi pupita wote wa siku zake, alivumbua kilichokosa maisha ya mwanadamu ili kukamilika. Baada ya miaka mingi ya kusaka, kufanya utafiti na mazoezi, yeye alikiri:

Mhubiri 12:13-14.

13Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

14Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

 

Huyu ni mfalme aliyekuwa ameweza kupata utajiri na kuimarika kimali ulimwenguni huu tulio kuliko mwingine yeyote. Alikuwa na dhahabu, fedha sio haba, mawe ya dhamana, ikulu sio haba, mashamba ya fahari, vidimbwi vya maji, wanyama, farasi (waliokuwa takriban elfu kumi na mbili) magari ya farasi na waendeshaji (takriban elfu moja mia nne). Michongo na mijengo ya ikulu yake na kiti chake cha enzi vilitia hofu. Mkusanyiko wa vitu vya kisanaa alivyokuwa navyo, hakukuwa na vingine duniani. Pia alikuwa na vijakazi wa kiume na wa kike maelfu waliofanyika kuwa wacheza vinubi, zeze na ala nyingine za muziki kumtumbuiza yeye. Pia alikuwa na wake zake mia saba, suria wake mia tatu kutoka mataifa tofauti na mila tofauti. Kumaanisha kuwa ilmbidi Suleimani kutangamana na mmoja wa wakeze, kila siku, mara moja tu kwa miaka miwili ili awe na wote angalau mara moja tu kwa miaka miwili. Kwa hivyo waona, kama ni kuimarika katika maisha ya kimwili, hadi siku tulizo, hakujawahikuwa na mmoja kama Suleimani, aliyekuwa na uimarifu wa kimali.

Zama zile, kupaa na kukwezwa hadi kuwa mfalme wa milki kama Israeli ilikuwa ni kama kuwa Mungu kati ya wanadamu, kwa sababu yeye alikuwa na nguvu zisizo kifani, bila yeyote wa kuzipinga kama ilivyo siku hizi katika serikali za kidemokrasia zenye vyama vya upinzani. Zaidi ya haya, Suleimani mwenyewe alikuwa amekirimiwa hekima ya kiwanadamu kupita kiwango cha wengine wote waliokuwemo zama zile. Kutumia hekima hii, Suleimani aliweza kutawala na kueneza milki yake juu ya ufalme wa Israeli wakati ambao kulikuwa na amani ambayo haingewezekana wakati mwingine wowote katika historia ya Israeli. Kutokana na hekima yake, alipata umaarufu kwa kukata kauli na kesi zilizowashinda wengine, akaandika zaburi na mafumbo, mashairi, na nyimbo zilizowavutia wengi waliozisikia kutoka tabaka na mataifa mengi ulimwenguni. Hekima yake iliyopita vipimo vya wakati ule, utajiri wake na ukarimu wake ulivutia umaarufu mwingi kwake na pia kwa milki ya Israeli.

Kuona kuwa moyo wa mwanadamu umesitirika katika kutafuta na kupata utukufu wa ulimwengu huu, na kuwa kufaulu ulimwenguni huu kwapimwa kwa kile mwanadamu anawezajivutia kwake, twawezasema Suleimani basi alikuwa amepata vyote katika hali hii. Katika haya yote, ukimtazama Suleimani kwa nje, wawezafikiri alikuwa mfalme aliyetimilika na kutulia katika hali zote za maisha yake, lakini haikuwa hivyo. Kitabu cha Mhubiri chapatiana hali ilivyokuwa katika fikra zake Suleimani na vile alivyoyaona maisha yake kwa kifupi. Inaonyesha kuwa hakupata kutimilika kwa kweli kwa kuwa angesema: “Sitapungukiwa kitu”. Lakini katika utukufu wake wa kilimwengu, Suleimani alipitia magumu, uchungu mwingi, na hali isioisha ya kutamani vingi na vingi zaidi. Alitafuta vyote vilivyoweza kutafutwa. Alijaribu iwezekanavyo tupata vyote vilivyowezapatwa ili kutuliza hamu ya kilimwengu, lakini hakuwezafikia hatima ile. Baadaye aliandika:

 

Mhubiri 1:8.

8Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

Kutosheleka kwa kweli na kukamilika ni sawa na utulivu, kitu ambacho kitaendelea kuwakwepa wengi wa kizazi hiki, kwa sababu moyo wa mwanadamu hautoshelezeki. Wawezaufananisha na kaburi ambalo haliwezishiba mizoga na mifupa ya walio wafu, ama jangwa ambalo huwezi kulinywesha maji likashiba, ama utumbo wa uzazi tasa ambao wapokea kila wakati lakini hauwezitunga mimba, na pia moto uendeleao kula kilicho mbele yake lakini hauzimiki wala kutosheka.

Mithali 30:16.

16Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isioshiba maji; na moto usiosema, Basi! 

Huu ndio ubatili wa kila mwanadamu anayeishi katika hali za chini kwa chini za huu ulimwengu tuliomo; kazi zao zote na kiu yao ya kutoshelezwa itakuwa sio kitu ila ubatili. Wataonekana ni kana kwamba wakaribia katika ukingo wa bahari kuu, lakini inawakwepa. Suleimani aliyajua yale pia, alikuwa amekagua na kujua mengi lakini akajua pale mwisho kuwa hili lilikuwa bure na mzunguko tu wa miviringo isiyoisha iliyomchosha tu yeye bila mwisho wake. Baada ya kutafakari kwingi alikiri: Utafiti, utunzi, vitabu vingi; na kusoma sana kwachosha mwili...yote yamekwisha sikiwa; hii ndio jumla ya maneno, Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. (Mhubiri 12:12-14). Hili akasema ndilo tu jambo la maana katika ulimwengu tuliomo na hata kizazi kijacho.

Suleimani alipata ufunuo fulani wa ufunguo uliokosa ili kuujaza uhai wa mwanadamu ulio na pengo la upweke. Kama mwanadamu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni, Suleimani alikuwa akiutafuta ufunguo wa kukusanya utajiri na umaarufu kwake mwenyewe, lakini kama inavyoonekana, mambo aliyoyapata hayakuwa na suluhisho lolote.Aliutafuta ule ufunguo katika wake wengi aliokuwa nao, na suria aliowakusanya kwake yeye, lakini hakuupata pale. Baada ya kuyawaza yale tena na tena, alifikia hatima na kusema kuwa yote hayo ni ubatili, bure na yasiyo dhamani yoyote chini ya jua, na kwa hivyo akawa na kilio kwa ajili ya ubatili waliotiwa wanadamu wa ulimwengu huu tulio. Lakini katika kufuatilia kumcha Bwana na kutii sheria yake Mungu, mwanadamu atavumbua utimilifu wa kweli anaoutafuta.

Kwa kweli, kutokana na machache tujuayo, Suleimani hakufikia hatima ya yale aliyokuwa akitafuta, kwa sababu, la kwanza, hakupata ufunuo kuhusu ile sheria ya Bwana aliyoizungumzia.

MANUFAA YA KUIFUATA SHERIA

Ili tukaweze kuelewa alichomaanisha Suleimani alipozungumzia kuhusu kumcha Bwana na kuifuata sheria yake, itatufaidi kurejelea ile mistari ya kwanza kwanza ya sura ile ya mwisho ya kitabu cha Mhubiri. Katika ile sura ya kumi na mbili, yeye aanza kwa kusema: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”. Aendelea kupambanua hatua kwa hatua vile uharibifu humwanzia mwanadamu anapoelekea kaburini anapomsahau Bwana Muumba wake. Siku ile, nguvu na uzima wa mwili alio nao kijana hudidimia, nazo siku za kuimba katika vilele vya upeo wa Sayuni hufanyika utupu na kuwa kiwiliwili cha mambo yasiyowezatimilika. Ni kama ndoto nzuri iishayo anapoamka. Wakati ule ndio ile nyota ya asubuhi ing’aayo na lile wingu lake Mungu linapotoweka machoni mwake, na macho na masikio kudidimia katika nguvu zao za kumpambanua Aliye Hai na hali ile takatifu Aliyo.  Wakati huo ndio ile chemichemi ya Maji ya Uzima inapofanyika kitu kisichowezafikiwa naye mwanadamu kwa sababu kiriba chake sasa hakina uwezo wa kuteka na kufifadhi yale Maji ya Uzima. Wakati ule ambapo mwanadamu analala katika kitanda chake katika kaburi la mavumbi, mahali ambamo hakuna hekima wala ufahamu wowote wa maarifa yake Bwana.

Haya yote yazungumzia kuhusu vile mwanadamu anavyopoteza maarifa ya utukufu ulio ndani mwake anapojikabidhi na kujinyenyekeza kwazo sauti za vilindi vya chini kwa chini vya mavumbi yaliyo chini mwake (ambayo ni ile hekima na maarifa ya kiwanadamu). Nalo kaburi pale lafanyika  hali ya tumbukio la wafu (kuzimu) ambao wapoteza maarifa ya Mungu wa kweli na wa Upendo, Ambarikiye mwanadamu na kila aina ya Baraka katika roho. Akiongozwa naye Roho wa Mungu, Suleimani aliianza ile sura yake ya mwisho ya Mhubiri kwa kufunua mwanadamu anavyondondoka kutoka hali yake ya utukufu na uridhi katika Mungu kwa njia ile ya kusahau au kwa maneno mengine, kupinda kutoka Mungu Muumba wake. Bwana Muumba wake ndiye asemaye, “Zaidi Yangu hakuna mwingine”:

Isaya 45:5-6.

5Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;

6ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.

“...Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine...” Yeye ndiye pia Asemaye, Ufunuo 1:18, “..na Aliye Hai...”

Kutokana na yote haya, ni bayana kuwa kunaye Mmoja tu Aliye Hai, Bwana pekee; aliye hai mwingine anao kwa sababu Bwana Yu Hai. Kuishi nje ya Ukweli huu ndio maana ya kifo. Yatazame maneno haya aliyoyasema Yesu:

Yohana 6:57.

57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, name ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.

Yeyote aishiye anaishi kwa ajili ya jina la Bwana; chochote kingine isipokuwa hicho ni kifo. Kumsahau Bwana ni kusahau hali yako isiyoonekana ya kweli na isiyo na uharibifu, hali ing’aayo kutoka milele. Hii yaashiria usingizi mkuu ambao mwanadamu huingia na kutembelea kimakosa katika mwili, akijidanganya mwenyewe kwa kufikiri kuwa yeye ni mwanadamu tu wa kijinsia na kuwa yeye ni kama wale wanyama waishio nyikani wakiwa na uambatanisho wa maisha yao na hali ya ulimwengu huu na kutoutilia maanani umuhimu wa milki aliyoundwa nayo ndani mwake toka milele. Mwanadamu, haujui kuwa Bwana wa Utukufu ndiye Uhai wako?  Haijaandikwa kuwa...Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na nyinyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu [Wakolosai 3:4]? Kwa maneno mengine, kufunuliwa Kwake ndiko kufunuliwa kwetu; ndiko kufunuliwa kwa hali yetu dhahiri kutoka milele. Huu sio muda wa maombolezi, kujionea huruma wala kunuguna, ila ni muda wa kusimama wima na kupokea ushuhuda toka juu unaoshuhudia kuhusu hii hazima ya dhamana iliyofichika katika hema hii yetu ya kimwili. Pokea maneno haya bure na kwa furaha na ukawezekubali yakuongoze toka hali ya kaburi ambamo uharibifu, dhambi na kifo chatawala kweli. Kumbuka mahali pako kati ya sayare na mawingu yanayong’aa ya mbingu. Tubu kusahau kwako na ukatamalaki tena kikamilifu. Ng’aa tena kama ile nyota ya asubuhi ambayo uliyo; amka na ukwee kwenye vilele vya Sayuni, na wimbo mpya wake Bwana Mungu wako.

Sura ya mwisho ya kitabu cha Mhubiri yaanza na “mkumbuke Bwana” na kuishia, “mche Mungu na uziti sheria zake”. Suleimani asema kuwa, kama mwanadamu atahifadhi kumbukumbu yake Bwana ambayo ni sawa na kuzitii sheria zake, yeye hatauona uvuli wa mauti na kaburi, mahali ambamo wanaomsahau Bwana hutupwa [Zaburi 9:7].  Mwanadamu mwaminifu atakuwa milele amelindwa tokana na masikitiko na laana ziwapatao watu wa kizazi hiki ambamo wana wa kiroho wake Adamu aliyeasi wamezikwa katika uasi wao.

NIMEKUJA KUITIMILIZA SHERIA

Swali kuu katika vinywa vya kila mwanadamu ni, tutawezaje kumhofu Bwana na kuzitii sheria zake, ili tujitwalie Milki hii Yake maridadi? Wayahudi walijua kuwa kulikuwa na umuhimu na manufaa ya kutii sheria  na ndio maana walikuwa na sherehe na mipangilio tofauti tofauti imeongezwa katika kuzikariri zile sheria za Musa n.k. Wangine wao wazikariri sheria za Musa na Zaburi kila siku wakisaka kujiweka wakfu na kumlenga Mungu na sheria zake pekee. Katika kule kujaribu kuitii ile sheria, wengine wameinyenyekeza miili yao kwa kufunga kwingi, kujikana vyakula Fulani na vinywaji, vyote hivi katika tumaini ya kujitwaalia mahali hapa palipokwezwa. Wengine wakajiweka katika hali ya upweke; wengine wakiwa watunga dini kwa nje n.k. Na kwa kuviangalia vitendo hivi, hakuna hata kimoja kimefaulu kumsongesha mwanadamuhatua hata moja kuukaribia ule utulivu wa Edeni ambalo lile shamba liliashiria na kuwakilisha. Wengine waliiona hii hali kwa mbali lakini hawakuwezi ishi ndani mwake; walitunga dini kupitia lile ndogo waliloliona. Watu wenye utimilifu wan je wamekuja na kwenda, lakini ukiyaangalia mambo kwa undani, hakuna yeyote Yule aliyepata kujitwaalia ile hali kikamilifu, ambayo Yesu asema imeandaliwa mpendwa wake.

Inadhihirika zaidi na zaidi kuwa jibu la kumcha Mungu na kuitii sheria yake liko ndani zaidi kuliko tujuavyo. Hata ingawa kuna shauku la kuivumbua tena Paradiso yake Mungu, na kuwa kuna ushuhuda ndani mwake mwanadamu unaomwambia kuwa lazima kuwe na unjia Fulani uelekeao katika fuarha hii isiyotamkika, mahali pa pumziko, raha milele katika utulivu, mwanadamu bado hana lile jibu. Katika sura ya ishirini na nane ya kitabu cha Ayubu, Ayubu anena kuhusu hali na milki hii, mahali ambamo giza – ambalo ni upumbavu wa kiroho hukomea na mwanadamu anaanza anatambua tena hali yake tukufu ya Edeni.

Ayubu 28:1, 3, 4-6.

1Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo...

3Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu.

4Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.

5Kama ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.

6Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.

Swali ni hili, unjia huu wa Uhai hupatikana wapi? Roho Afunua kupitia Ayubu kuwa unjia huu uelekeao kwenye upambanuzi wa Nuru umefichwa machoni pa wanadamu wa ulimwengu huu. Vilindi vya bahari, kifo na uharibifu, ambazo ni viashirio vya ulimwengu tulio, mahali ambamo wanaomsahau Mungu hupatikana, una fununu tu za mahali hapa paitwapo Paradiso lakini ni dhahiri kuwa bado ni fumbo kwa ulimwengu.

Ayubu 28:13-22

13Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai.

14Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu;...

22Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.

23Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.

Kwa haya yote ni bayana kuwa hii hali ya dhamana imefichika kutoka kwa mwanadamu wa ulimwengu huu aliyelala katika kitanda chake kuzimu. Hata Suleimani mfalme katika utukufu wake wote wa kilimwengu, alikuwa kwa kweli ni mmoja tu wa wale walioko katika hali hii ya chini kwa chini ya walio wafu. Katika utukufu wake wa kilimwengu, anabaki chini ya wale wanaovumbua mahali hapa pa Uzima. Ni kweli, yeye aliandika makuu namengi, alikuwa mwenye hekima zaidi kuliko wote ulimwenguni huu tulio, lakini wakati ule, hakupewa uweza wa kuona kwa kweli na pia kuelewa kuhusu mambo aliyoyaandika. Sura ile ile ya ishirini na nane ya Ayubu yaishia kwa suluhisho kama lile lake mfalme Suleimani inapokiri kuwa ule unjia wa kuingia hazina hii ni katika kumhofu Bwana na kuuondokea uovu. Niulize tena, tutamweka vipi Bwana katika ukumbusho, kumhofu Yeye, kuzitii sheria zake na kuuondokea uovu? Lazima kuwe kimsingi ufunuo toka juu; sauti kuu igurumayo na radi iwakayo toka mbinguni Kwake Baba wa Nuru ndani ya mioyo ya waishio vilindini – ulimwenguni. Ni karama kutoka kwake Mungu.

Ayubu 28:23-28.

23Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anaijua mahali pake.

24Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima.

25Apate kufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.

26Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.

27Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

28Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Ngurumo na umeme wa radi ndio ile sauti toka juu isemayo, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye”. Ndio ile ile sauti ingurumayo toka mbinguni katika moyo wake Petero na kumfanya yeye kuyakiri maneno ya siri: “Wewe ndiwe Kristo (Mpakwa Mafuta wake Mungu bila kipimo), Mwana wa Mungu aliye hai”. Ufunuo wa Mwana wa Mungu ambao ulimpotelea mwanadamu, ndio njia ya kumhofu Bwana na kuuondokea uovu ambayo humwongoza mwanadamu kurudi katika utukufu wa siku za ujana wake, kurudi milele mahali ambamo Uhai wa Kweli umo na vilele vyake. Kwa kupiga ngurumo masikioni mwetu na kutia nuru machoni mwetu kupitia umeme wa radi, Baba hutupa ufunuo wa siri ya Mwana wa Mungu ili tusiweze tena angamia  katika kaburi la wanadamu ila tuweze tena kupaa kurudi kwenye mahali pa Uzima.

Yohana 3:16 Kwa jinsi hii Mungu aliupenda ilumwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Kwa ajili ya Upendo wake kwetu, Mungu kupitia UFUNUO WA KUFANYIKA MWILI KWA UPENDO ameamuru Nuru yake kuangaza ndani ya mioyo yetu ili kufunua siri zilizofichika za Mwana wake Mungu. Huu Uzima wa milele ni Uhai wa Mwana wa Mungu ambao Suleimani anauzungumzia kama ‘siku za ujana wake’. Siku ambazo unaangaza na miale Nuru safi kama Aliyokuwa nayo Yesu alipogeuzwa kwenye vilele vya Sayuni, na ya Alfa na Omega – Yule Mkuu Aliyekwezwa palipo Juu Zaidi Pa Mungu.

Ufunuo wake Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu umekuja kama umeme wa radi kumfanya mwanadamu mara tena kutimiza sheria na akaweze kuishi. Dini yako, iwe imeanzishwa naye Musa au nabii mwingine yeyote haiwezikusaidia kutimiza hitaji msingi la kumhofu Bwana na kutii sheria zake. Hata zile imani na shauku ulizo nazo – haziwezi kukuvuta kumsogea Yeye Mungu wala ulimwengu wake. Kile tu kinachohitajika ni ufunuo wa Mwana wa Mungu; Hii ndio njia kurejea Utukufuni wa Baba.

Kama umeme wa radi na ngurumo toka mbinguni juu, ufunuo wa Mimi Ndiye – Kristo Aliye Ndani, Mwanzo wa kuumba kwa Mungu, Aliye Mtakatifu, Amekuja kumfanya mwanadamu kuweza kutimiza sheria: 

Mathayo 5:17.

17Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

Kufunuliwa kwa Mimi Ndiye – Kristo Aliye Ndani, Bwana wa Utukufu, kumeja kurejesha utajiri wa uhai wa Edeni:

Yohana 10:10...Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kasha wawe nao tele.

Ufunuo wa Kristo Aliye Ndani ni matendo na kazi yake Baba, kuleta uponyaji kwake mwanadamu, kuikweza nafsi yake kutoka kifo, mauti na uharibifu ili kumkirimia taji la Uzima. Huu ufunuo warejesha nguvu zangu za ujana mara tena, kunifanya mie kupaa katika vilele vya Sayuni na kelele za shangwe.

Zaburi 103:1-5.

1 Zaburi ya Daudi. Ewe nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.

2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.

3Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,

4Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,

5Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;

Ni ufunuo wa Mimi Ndiye – Kristo Aliye Ndani unipeao ushindi thidi ya dhambi, mauti na kaburi, ili nikawezekutembea katika ushindi wa pekee, katika uhuru wa Mwana wa Mungu.

1Wakorintho 15:55-57.

55Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

56Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.

57Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tokana na haya yote, ni dhahiri kuona kuwa kujaribu kuambatana na miigo, tamaduni na sheria za ‘tenda hili – usitende lile’, tukidhania kuwa kupitia yale tunampendeza Mungu, ni utupu tu. Kumcha Mungu na kuzifuata sheria yake inakamilishwa katika kupata ufunuo wa hii siri ya Mwana wa Mungu na kuihifadhi ile. Baba ametupa Roho wake leo ili tuweze kikamilifu kuelimishwa kuhusu Mwana wa Mungu tulio sisi, kibinafsi na kijumla. Tunapopata picha ile pananuzi, ya umahiri wa hali yetu isiyoharibika nay a milele ya Mwana Aliye Ndani, sis twafunguliwa kutoka kwa ngundi ishikamanishayo wana na uharibifu unaotamalaki ulimwenguni. Uhuru kutoka kwa tama zinazochafua nafsi zao wanadamu kwa sababu ya upumbavu uliositirika ndani ya mioyo yao wapatikana kwa kulikumbatia hili funzo la Siri ya Kristo Aliye Ndani.

TORATI TOKA MWANZO

Kuitii sheria ya (za) Mungu na sawasawa na kumcha Mungu; ni yote hayo yamewekwa kimsingi katika kuijua siri ya Bwana katika Kweli. Kama mwanadamu awaye yeyote atalipenda Jina la Bwana, yeye atazitii sheria za Bwana; na huu ndio Uzima wa Milele. Kumpenda Bwana ni kule kujijua na kuwajua ndugu katika Kweli. Kuanguka kutoka kwenye hili ndicho kifo. Hii ndio ile Ishara ya Zama Zile ambayo haipaswi kusongeshwa. Mtume Yohana azungumzia  kuhusu sheria itokayo mwanzo nah ii sheria imekuja kwetu tena kama Nuru iangazayo kwenye giza la njia zetu za kale za kimwili ili kutupa ufunuo wa Yule aliye Hai Ndani ya kila mmoja wetu. Huu ni ufunuo wa Umoja ukitangaza kuwa MUNGU NI UPENDO, na kila aliyezaliwa, kuumbika au kutungika naye Mungu hupenda. Haisemi kuwa, kila mmoja aliyezaliwa na Mungu HUJARIBU kupenda, ila yasema, kila azaliwaye na Mungu HUpenda, kwa sababu hi hali yake ya kawaida kufanya vile. Sheria ni kuwa ...tujihifadhi katika Umoja wa Roho katika kifungo cha amani...kwa sababu tu Mwili Mmoja. Yesu hakuja kutufanya Mwili Mmoja, ila Alikuja kufunua kuwa sisi Ni Mmoja; na Huyo Mmoja Ni Mungu Pekee na Uzima wa Milele (1 Yohana 5:20).

Hakuna tunachowezafanya kama wanadamu duni kifanyikacho katika haya maisha kinachowezaharibu huu Umoja. Hauwezivunjika hata milele yote. Mwanadamu kama hana fahamu za huu Umoja, yeye ako katika sehemu za nje  kunako giza na huugua mambo mengi yasiyofaa na ambayo humtumbukiza katika uharibifu asiouhitaji na usioisha. Utengano kati ya ndugu huundika tokana na kuwa ufahamu wa wanadamu hutiwa giza ili wasiweze kuutambua Mwili wa Bwana uwajaao wote ndani ya vyote. Hekima ya ulimwengu huu unaotokana na fikra za kimwili huwafanya wanadamu kutenda kazi zisizoambatana na fikra za Mwili wake Mungu. Kwa hilo, twahimizwa tuondokee giza la ulimwengu huu, kwa sababu yote haya ni ya kilimwengu na ni tama za macho, tama za mwili na kiburi cha maisha. Hisia hizi za kishetani ziundwazo kupitia karakana za ulimwengu huu huuficha ukweli wa Mwili wake Mungu tokana na macho ya mwanadamu, na ndio chanzo cha uovu rohoni tunaouona ulimwenguni wa sasa. Mwanadamu yeyote akiupenda ulimwengu huu tulio, Upenda wake Mungu haumo ndani yake, na kwa hiyo ahitajika kuuacha ulimwengu huu wa sasa na tama ziambatanazo nao ili awezevumbua Ulimwengu wake Mungu – Milki Yetu.

Kwa nini utamani na kutafuta utukufu batili? Hujui kuwa dunia na vyote vilivyomo ni vyake Bwana; hauelewi kuwa vyote ni vyako? Hekima, Utukufu, Ukuu, Nguvu, Mamlaka vyote vimo ndani Mwake Mtakatifu wa Mungu milele yote. Amka ndani mwake na utambue kuwa Mimi Ndiye Yeye. Kupigania mali na utukufu wa ulimwengu huu kwajumlisha tu masononeko; simama wima na ujue kuwa vyote ni vyako. Jivike jicho lako la kiroho na ukawezefurahia vyote; ni vyako kutumia kwa kutumbuika kwako. Usiseme, “Nahofu”, wala usiulize, “Nitala nini na nitajivika nini” kwa sababu Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa, tulia tu na uliamini Jina Langu name nitazifanya ndoto zako za Utukufu kutimia.

 Tena, sheria ile ya kale na ya kwanza imerejea kama sheria mpya kwa sababu upumbavu wa Umoja wetu dunia nzima katika Yule Aishiye wadidimia na kupita, wakati ambapo ufunuo wa Kristo wapambazuka katika mwanadamu.

1Yohana 2:7-9.

9Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilosikia.

8Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yenu; kuwa giza linapita na nuru ya kweli imekwisha kung’aa.

9Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.

Upendo ndio sheria, na Mungu Ni Upendo; Mungu Ndiye Aishiye, Mungu juu ya Yote, Ndani ya Wote, na Ndani Yetu Sote. Na hili funzo la upendo likaweze kumwinua kila mwanadamu toka vilindi vya maji kurejea tena katika vilele ndani mwake Mungu, ambamo utavumbua furaha na amani ambayo ulimwengu huu haujafahamu bado. Mwisho wa imani ni kuvumbua tena utajiri wa kweli wa Uzima ambao umemkwepa mwanadamu miaka na mikaka na hili huja kwa kuukubalisha huu ufunuo wa Upendo na Umoja kutuongoza tena kurejelea huyu mtu ambaye katika yeye, Utimilifu wa Mungu waishi kimwili. Tega sikio Ewe Israeli, Bwana Mungu wako Ni Mmoja. Unayo masikio ya kuyasikia haya? Wasikia asemacho Roho? KunayeMmoja, na Ndiye Bwana Mungu wako – na Yumo Ndani yake nay a jirani yako. Kwa hiyo, mpende Mungu wako na moyo wako wote, na jirani yako kama ujipendavyo wewe mwenyewe. Kuamka ili kurejea katikahii hali ya Umoja wa kiungu ii zaidi ya ufahamu wa mwanadamu na ndiyo ufunguo wa kuingia katika raha na utimilifu wa kweli. Umoja katika Bwana ni ufunguo kutoka kuzimu na kifo kurejea Paradiso. Hofu ya Bwana na kutii sheria yake takatifu ya Umoja huja kwa Ukumbusho wa Bwana Aishiye; Yeye Yu Ndani mwenu nyote.  

Nitamalizia na maneno ya wimbo uitwao ‘Nature Boy’, wake Nat king Cole. Huyu alikuwa ni mtu wa hekima aliyetembea juu chini, huku na kule akitafuta ufahamu; baadaye alitambua kuwa Upendo ulikuwa ndicho kitu cha dhamana zaidi alichopata.

Kulikuwa na kijana, kijana wa kustaajabisha sana.

Walisema alitembea mbali, mbali sana kuvuka mabonde na bahari.

Mwenye haya na huzuni machoni lakini hekima alipewa.

Na siku moja, siku ya maajabu akanipitia

Na tuliponena mambo mengi, wapumbavu na wafalme

Hili akaniambia

“Jambo kuu mno utajifunza

Ni kupenda tu na kupendwa pia”

 

 

Baraka Kwenu.

Trevor & Emiemineni Eghagha